Habari

Katibu Mtendaji wa TNBC Dkt. Godwill G. Wanga akutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru CP. Salum Hamduni baada ya Mkutano leo tarehe 25.01.2023
  • 25 Jan, 2023
Katibu Mtendaji wa TNBC Dkt. Godwill G. Wanga akutana na kufanya mazungumzo na  Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru  CP. Salum Hamduni baada ya Mkutano leo tarehe 25.01.2023

Katibu Mtendaji wa TNBC Dkt. Godwill G. Wanga akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru  CP. Salum Hamduni baada ya Mkutano kujadili namna ya kuzuia rushwa ili isiathiri mazingira ya biashara na uchumi Nchini. Mkutano huo umefanyika leo tarehe 25 januari 2023 Jijini Dar es Salaam. Viongozi hao wamejadili namna ya kuwajengea uwezo Wafanyabiashara na Wawekezaji Nchini kutojihusisha na rushwa. aidha, Wakuu hao wamepongeza Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa TNBC kwa jitihada mahsusi za kuzuia rushwa Nchini. Kazi Inaendelea.