Tanzania National Business Council

VIKUNDI KAZI VYA TNBC (Working Groups )

Katibu Mkuu Kiongozi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati Tendaji ya Baraza la Taifa la Biashara (TNBC), Mhe. Balozi John William Kijazi amezindua Vikundi Kazi vya Baraza kwa lengo la kujenga na kuimarisha mahusiano kati ya Sekta za Umma na Sekta Binafsi katika kuibua changamoto na kuzijadili kwa mustakabali wa maendeleo ya Tanzania. “Lengo la kuanzisha Vikundi Kazi hivi ni kufanya interactions za kitaalam zaidi. Vikundi kazi hivyo ni Kikundi kazi cha Kilimo (Agriculture Working Group), Kikundi kazi chaViwanda (Industrialization Working Group), Kikundi kazi cha Misitu (Forestry Working Group), Kikundi kazi cha Mazingira ya Biashara (Business Environment Working Group), na Kikundi kazi cha Utalii (Tourism Working Group). Kila Mjumbe wa Kikundi Kazi ana majukumu muhimu hivyo kuwepo kwenu kumedhihirisha upendo wa kulitumikia taifa letu. Vikundi Kazi hivi vitakutana Kisekta mara kwa mara na muundo wake ni Wajumbe 50 toka Sekta ya Umma na Wajumbe 50 toka Sekta Binafsi. Vikundi Kazi vitakuwa na Mwenyekiti kutoka Sekta ya Umma na Mwenyekiti Mwenza atatoka Sekta Binafsi.”

Kikundi kazi cha Kilimo

Kikundi Kazi cha kilimo, kinahusisha  Wafugaji, Wakulima na  Wavuvi, ni Sekta inayo ajili wengi. Kikundi Kazi hiki kinatakiwa kufanya ufuatiliaji na tathimini ya utekelezaji wa nguzo kuu za Kilimo Kwanza ili baadaye yatolewe mapendekezo yautekelezaji wa haraka wa mpango wa kuendeleza Sekta ya Kilimo awamu ya pili yaani ASDP II ambao ulizinduliwa na Mheshimiwa Raisi hivi karibuni. Kikundi Kazi bado kinajukumu la kwenda kuchambua ilikuona ni maeneo gani Serikali na Sekta Binafsi zinatakiwa kufanyia kazi zaidi.

Kikundi Kazi cha Viwanda

Serikali inaendelea kuondoa changamoto mbalimbali za Sekta ya maendeleo ya Viwanda nchini. Taasisi za udhibiti kama vile TBS na TMDA sasa hivi zinafanya kazi pamoja. TBS wameanzisha kanda tano nchini ambazo ni Kaskazini,Kusini, Nyanda za juu kusini, Kanda ya Ziwa na Kanda ya Kati ili kusogeza huduma kwa Watanzania wote.

Wazo la kuanzisha Kikundi Kazi cha Viwanda lilitoka kwa Sekta Binafsi katika kikao cha 10 cha Baraza la Taifa la Biashara kwamba iundwe kamati ya viwanda ya kitaifa. Kwa hiyo, Kikundi Kazi hiki ni muafaka na kina wataalamu, wenye uwezo wa kuchambua mambo na kutoa mapendekezo yenye weledi wa kuwezesha sekta ya viwanda kwenda mbele.  Tunategemea kikundi hiki kitakuja na mapendekezo yatakayowawezesha Watanzania wote na Wawekezaji kutoka nje  kushiriki kikamilifu katika kuifikisha nchi yetu katika uchumi imara wa viwanda.

Kikundi kazi cha Misitu

Rasilimari ya misitu imekuwa haitumiki ipasavyo (underutilized) siku za nyuma. Ni muhimu kutambua kuwa raslimali ya misitu ni kichocheo muhimu katika kukuza ajira na uchumi wa viwanda vya kutengeneza bidhaa zitokanazo na misitu na kutunza au kuhifadhi mazingira endelevu. Ni mategemeo ya TNBC kwamba wajumbe wa kikundi kazi hiki cha Misitu wataleta mapendekezo na ushauri ili yafanyiwe kazi haraka iwezekanavyo kwa maendeleo ya nchi yetu Tanzania.

Kikundi kazi cha Mazingira ya Biashara

Kikundi kazi hiki ni muhimu sana kuboresha mazingira ya biashara ili kuvutia uwekezaji na biashara nchini Tanzania. Uboreshaji wa mazingira ya biashara huongeza ufanisi na tija ya rasilimali zilizowekezwa na hivyo kuchangia kukuza uchumi wetu. Masuala muhimu yanayohusu mazingira ya biashara ni pamoja na miundombinu yote, upatikanaji wa ardhi na mitaji, utoaji wa vivutio, punguzo la kodi na tozo zisizokuwa na tija, sera na sheria rafiki kwa biashara na uwekezaji, na kadhalika. Kikundi kazi cha kuboresha mazingira ya biashara kinapaswa kutafiti, kuainisha, na kutoa mapendekezo ya maboresho kuhusu masuala yote yanayoathiri biashara na uwekezaji Tanzania.

Kikundi kazi cha Utalii

Kikundi kazi hiki cha utalii kitajikita katika kuvutia na kuboresha utalii nchini Tanzania. Sekta ya utalii ni chanzo kikubwa cha fedha za kigeni na ambacho kina mchango mkubwa wa kujenga uchumi stahimili na uliotulia. Hivyo, Kikundi kazi hiki kiainishe chanagamoto na kitoe mapendekezo ya mikakati mahsusi itakayohifadhi utalii na itakayovutia watalii wa ndani na nje ya nchi kutembelea na kufurahia fursa zote za utalii nchini Tanzania.

Comments are closed.