Habari

Dkt. Godwill Wanga, Katibu Mtendaji, TNBC akutana na kufanya mazungumzo na Bw. Deogratius Massawe, Kaimu  Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF katika Ofisi za TNBC
  • 23 Oct, 2025
Dkt. Godwill Wanga, Katibu Mtendaji, TNBC akutana na kufanya mazungumzo na Bw. Deogratius Massawe, Kaimu  Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF katika Ofisi za TNBC

Dkt. Godwill Wanga, Katibu Mtendaji, TNBC amefanya mazungumzo na kumkabidhi nyaraka muhimu Bw. Deogratius Massawe, Kaimu  Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF, kwa ajili ya kuimarisha mahusiano ya kiutendaji na Mikutano kati ya sekta ya umma na sekta binafsi (PPDs) kuhusu uboreshaji wa mazingira ya biashara na uwekezaji ili kuendeleza ukuaji wa uchumi Tanzania. Tukio hilo limefanyika leo tarehe 23 Oktoba, 2025 katika Ofisi za TNBC, Mtaa wa Ghana 21, Dar es Salaam. TNBC ni kiungo muhimu kati ya Sekta ya Umma (Mawaziri) na Sekta Binafsi (Wenyeviti wa Taasisi) chini ya uongozi mahili wa Mwenyekiti wake, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.