Habari

Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa TNBC aongoza Mkutano wa 15 wa TNBC
  • 30 Jul, 2024
Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa TNBC aongoza Mkutano wa 15 wa TNBC

Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa TNBC ameongoza Mkutano wa TNBC leo tarehe 29 Julai, 2024.

Mkutano wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC) ni jukwaa muhimu katika kujadili mazingira ya biashara, uwekezaji na uchumi kwa ujumla hapa nchini.

Kupitia mkutano huu amesisitiza agizo lake la kuhakikisha mifumo ya TEHAMA nchini inaboreshwa, inaunganishwa na kusomana ifikapo mwezi Disemba mwaka huu, ili kurahisisha utoaji wa huduma kwa wananchi kupitia mifumo ya kielektroniki na kuongeza kasi na uwazi katika utendaji kazi.

Amepokea maoni na mapendekezo toka kwa wafanyabiashara ambayo Serikali itayafanyia kazi. Sambamba na hilo, ametoa wito kwa sekta binafsi kuendeleza dhamira yake ya kufanya kazi na Serikali kama mbia na sio mshindani, ili kwa pamoja tuendelee kulijenga Taifa letu.