Habari
Majadiliano ya Kisekta, Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo
- 30 Mar, 2023
Mhe. Bal. Dkt. Pindi H. Chana Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo na Mwenyekiti wa ‘Ministerial Public Private Dialogue’ – MPPD leo tarehe 30.03.2023 ameongoza Mkutano wa Majadiliano ya Kisekta kati ya Sekta ya Umma (Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo) na Wadau wa Sekta Binafsi katika Ukumbi wa ‘VVIP’ katika uwanja wa Benjamini Mkapa Jijini Dar es salaam. Mkutano huo umehudhuliwa na Katibu Mtendaji wa TNBC Dkt. Godwill G wanga.