Habari

Tanzania Investment Facilitation Single Window System
  • 19 Jan, 2022
Tanzania Investment Facilitation Single Window System

Katibu Mtendaji - TNBC, Dkt. Godwill Wanga akiwa pamoja na Dkt. Maduhu Kazi, Mkurugenzi Mtendaji – TIC pamoja na Wataalam wa kujenga mfumo wa ‘Tanzania Investment Facilitation Single Window System’. Kazi hii inatekelezwa kwa mujibu wa azimio la Mkutano wa 12 wa TNBC  uliofanyika tarehe 26 Juni 2021 IKULU Jijini Dar es salaam ulioongozwa na Mwenyekiti wa TNBC Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Timu hiyo iko mkoani Morogoro na ujenzi wa Mfumo huo umefikia 42% na Timu imeahidi kukamilisha kazi hiyo mwezi Februari 2022. Kazi Iendelee.

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Tanzania Census 2022