Habari

TANZANIA - OMAN BUSINESS ROUNDTABLE 8 SEPTEMBER, 2025
  • 08 Sep, 2025
TANZANIA - OMAN BUSINESS ROUNDTABLE 8 SEPTEMBER, 2025

Dkt. Godwill Wanga, Katibu Mtendaji Baraza la Taifa la Biashara akiwasilisha kuhusu vivutio na maeneo mbalimbali yanayeweza kuwekezwa nchini Tanzania na Wawekezaji kutoka Nchini Oman katika kongamano baina ya Tanzania na Oman lililofanyika katika Hotel ya Kempiski Jijini Dar es salaam tarehe 8 Septemba, 2025. Kongamano hilo liliongozwa na Mwenyekiti wa Shirikisho la Sekta Binafsi Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti Mwenza wa Kamati Tendaji ya TNBC Bi. Angelina Ngalula na kufunguliwa na Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kikundi Kazi cha Viwanda, Dkt. Hashir Abdallah